Kwa wazazi wengi nchini Kenya ,kumlea mtoto mwenye usonji ,Autism ,si malezi ya kawaida ni malezi yenye mzigo mzito, gharama  na inanyanyapaisha. Carol Korir ametuandalia ripoti kuhusu namna shule moja nchini Kenya inawajumuisha wazazi kwenye elimu ya watoto wenye usonji.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa wazazi na walezi wa watoto hao, Siku zao hutumika kwenye ziara za kliniki za kutoa tiba  nasaha  ambazo huwa ghali  na kujaa unyanyapaa kutoka kwa jamii. 

Kwenye  Mali Integrated School, ambayo itakuwa ya kwanza  Afrika Mashariki mambo ni tofauti kidogo.

Hapa wanafunzi watapata masomo yanayoendana na mahitaji yao ,walimu wakitumia mbinu bunifu kama muziki kuwapa elimu.

Hao ni walimu wa muziki wanaowahudumia watoto hao.

“Wewe unamchezea tu jambo moja halafu anarudia kwa kukumbuka.” alisema mmoja wa walimu.

“Unahakikisha uko naye hapo kisha unamwonesha hii namna ya kushika.” alielezea mwalimu pia.

“Wengi wao tukiwachezea muziki wanatulia.” alisema mwalimu mwingine.

Mwasisi wa Shule hii Elizabeth Pauline Wamukowa ,anasema kilichomchea ni mtoto wake Daniel Mali  ambaye ana usonji, na  sasa masomo yake yako hatarini kwa kuwa hamna shule inayomfaa.

“Mimi hupenda kutumia mtoto wangu kama Compass kwa mfano saa hii  amefanya mtihani wa Gredi 6,wenzake wanaendelea na Gredi 7 lakini yeye amekaaa nyumbani,sababu shule ile yupo haiwezi kushughulikia mahitaji yake  kabisa ya kimasomo.” alielezea Elizabeth Pauline Wamukowa.

Shule hii maalum pia inazingatia wazazi na walezi ,mahali ambapo wanaweza kupumzikia  wanao pia wakishugulikiwa.

Hao ni baadhi kwa wazazi hao.

“Tunahitaji hata sehemu ya kulala kwa sababu wakati mwingine watoto wetu hawalali.” alisema mzazi mmoja.

“Sitahangaika kutafuta shule.” alisema mzazi mwingine kwa Jina Vanessa.

Shirika la afya duniani limebaini ongezeko la watu wenye usonji. Ongezeko hili likimanisha  uhitaji mkubwa wa matunzo maalum, na shule ya Mali ni moja ya ufumbuzi unaolenga kutatua changamoto hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *