Ajali za pikipiki maarufu kama bodaboda zimeendelea kusababisha madhara makubwa mkoani Mwanza, ambapo watu 33 wamefariki dunia na wengine 65 kujeruhiwa katika ajali 72 zilizotokea katika kipindi cha mwaka 2024/25.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Saida Mtanda amewataka waendesha bodaboda kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali hizo, huku akisisitiza umuhimu wa kujiunga na bima ya afya na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa ajili ya usalama wa maisha yao ya baadaye.

Pia amewataka wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo kukutana na waendesha bodaboda ili kuweka mikakati itakayowawezesha kunufaika na mikopo ya vijana pamoja na asilimia 10 ya mapato ya halmashauri, hatua itakayosaidia kuongeza mitaji na kuboresha maisha yao.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *