Ripoti ya Madaktari wasiokuwa na mipaka MSF, imebaini kuwa wafanayakazi wa ndani na wa nje, waliwanyanyasa wakimbizi nchini Chad, wakiwemo wasichana wenye umri chini ya miaka 18.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo ya ndani ya MSF inaeleza kuwa, wakimbizi hao walinyanyaswa ili kupewa chakula na wakati mwingine wanawake kutakiwa kushiriki ngono na wafanyakazi wa shirika hilo ili kupata kazi.

Utifiti huo ulikamilika mwezi Julai mwaka uliopita, lakini ripoti hiyo imetolewa wazi siku ya Jumamosi, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Associated Press.

Miongoni mwa wakimbizi walionyanyaswa ni mwanamke kutoka Sudan ambaye alinyanyaswa kingono kabla ya kupewa ajira.

Aidha, ripoti hiyo inaeleza kuwa visa 59 ya unyanyasaji vilibainika, huku wafanayakazi 18 wa MSF wakiachishwa kazi, huku wakimbizi walionyanyaswa wakiogopa kuzungumza.

MSF ni miongoni mwa mashirika makubwa yasiyokuwa ya kiserikali ambayi yanatoa huduma za kibinadamu katika kambi ya wakimbizi nchin Chad, kwa raia wa Sudan ambao wameyakimbia makaazi yao kwa sababu ya vita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *