Mhariri na Mtangazaji wa Radio Free Africa, Clara Matimo, ameingia miongoni mwa wanahabari waliotunukiwa Tuzo ya Umahiri wa Uandishi wa Habari za Hedhi Salama kutokana na mchango wake katika kuendeleza uelewa wa jamii kuhusu afya ya hedhi na haki za wasichana na wanawake nchini.
Kupitia vipindi, makala na taarifa mbalimbali alizozitayarisha na kuziwasilisha hewani, Clara Matimo amekuwa sauti muhimu katika kuibua changamoto zinazowakumba wasichana wakati wa hedhi pamoja na kuonesha suluhisho zinazowezekana katika kuboresha mazingira ya elimu na afya.
Tuzo hii ni uthibitisho wa juhudi zake katika kutumia vyombo vya habari kuleta mabadiliko chanya katika jami.

(Feed generated with FetchRSS)