Mfanyabiashara mbobezi wa masuala ya uchukuzi, usafirishaji na biashara za bandari ambaye pia ni Mkurugenzi wa MB KUU Group of Companies, Athumani Zuberi Mwesongo, amesema Tozo ya Maendeleo ya Miundombinu ya Bandari (PIDL) inayotarajiwa kuanza kutumika Julai 1, 2026 ni moja ya hatua muhimu za uwekezaji zinazolenga kuwezesha Tanzania kuendelea kuboresha na kupanua miundombinu ya bandari kwa viwango vinavyoweza kuhimili ukuaji wa biashara wa sasa na wa baadaye.
Amesema mataifa yaliyojenga bandari kubwa na zenye ushindani duniani kama Singapore na Uholanzi kupitia Bandari ya Rotterdam yalifanikiwa kwa kuwa na mifumo endelevu ya kufadhili uwekezaji wa miundombinu ya bandari kwa muda mrefu.
Mwesongo amesema bandari ndiyo ateri kuu ya biashara ya dunia kwa sasa, huku zaidi ya asilimia 80 ya biashara zote za kimataifa zikisafirishwa kwa njia ya bahari.
(Feed generated with FetchRSS)