Wataalamu wengi wa masuala ya siasa wametathmini utangulizi wa mapatano ya kusitisha vita kati ya Marekani na Jamhuri ya Kislamu ya Iran na kuyataja kuwa fedheha kubwa kwa utawala wa Marekani unaoongozwa na Rais Donald Trump.

Trump akishirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel walikuwa wameainisha na kutangaza hadharani malengo yao ya kuanzisha vita vya kichokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, muhimu zaidi likiwa na kupindua utawala halali wa Kiislamu wa Iran na hata kuutaka ujisalimishe mwanzoni mwa uchokozi huo, ambapo viongozi wa ngazi za juu wa Iran wakiongozwa na Kiongozi Mkuu pamoja na makamanda wa juu jeshini na wasomi wa Iran waliuawa kigaidi katika mashambulio ya mwanzoni mwa uchokozi huo. Pande hizo mbili hasimu zilidhai kwamba Iran ni tonge ambalo lingemezwa kirahisi bila kukabiliwa na gharama kubwa na matatizo ya kisiasa. Lakini baada ya kupita siku chache za mashambulio, mambo yalizigeuka na kujipata kwenye hali ngumu katika madeni ya vita huku kukiwa na taathira nyingi hasi za kiuchumi na kisiasa kwa pande hizo chokozi.

Kwa kuitilia maanani hali hiyo pande hizo zimekuwa zikitafuta sababu na visingizio mbali mbali vya kujikwamua na kujitoa kwa heshima kwenye kinamasi hicho cha kijeshi, na hata kuamua kuchukua hatua za kujidhalilisha kwa ajili ya kufikia lengo hilo. Kuhusiana na hio, gazeti la The Washington Post limeandika katika ripoti kuhusu mkataba wa Iran na Marekani kwamba Donald Trump sasa anasherehekea kurejea kwa hali iliyokuwepo kabla ya Februari 28; ambapo baadhi ya wataalamu wanaamini kuwa kiuhalisia ni fedheha kubwa kwa utawala wake na mshirika wake Benjamin Netanyahu wa Israel.

Maelewano ya awali ya kumaliza mapigano kati ya Iran na Marekani yamefikiwa huku Trump akijaribu kuhitimisha vita hivyo vyenye gharama kubwa kwa walipakodi wa Marekani licha ya majigambo na madai yake yasiyo na msingi mwanzoni mwa vita kuwa eti alikuwa ameharibu kabisa nguvu za kijeshi za Jamhuri ya Kiislamu, na hivi sasa anajaribu kufungua tu Lango-Bahari la Hormuz ambalo tayari lilikuwa wazi hata kabla ya kuanza vita.

Siku ya Jumapili, Trump alitangaza mwisho wa kampeni yake ya kijeshi dhidi ya Iran akisema: “Meli za dunia, asheni injini zenu. Acha mafuta yatiririke!”  Kulingana na mwandishi wa gazeti la Washington Post, Trump anasherehekea kurejea kwa hali iliyokuwepo kabla ya Februari 28, kabla ya mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

 

Ripoti hiyo inasema: Mapambano makali ya Iran katika miezi ya hivi karibuni, yameibua mpasuko mkubwa kati ya rais wa Marekani na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kiasi kwamba Trump amemkemea vikali mbele ya waandishi wa habari katika sehemu ya tafrija ya kusherehekea miaka 80 ya kuzaliwa kwake.

Sehemu nyingine ya ripoti hiyo inasema: Kinyume na matamshi yake kabla ya vita, rais wa Marekani hazungumzii tena kuhusu mabadiliko ya utawala nchini Iran na amejikita tu katika mazungumzo na Tehran na kujiepusha na hatua zozote za kijeshi zinazoweza kuhatarisha amani, kama tulivyoshuhudia siku ya Jumapili ambapo alimkosoa vikali Netanyahu kwa kushambulia mtaa mmoja wa Lebanon kinyume na mapatano ya usitishaji vita na Iran.

Gazeti la Washington Post limezidi kubainisha upinzani wa baadhi ya wafuasi wa Trump dhidi ya usitishaji vita na Iran, akiwemo mtangazaji wa redio na mchambuzi Mark Levin, ambaye ametaka kutangazwa hadharani maelezo ya makubaliano hayo.

Seneta Lindsey Graham, mtu mwingine wa karibu na Trump na muungaji mkono mkubwa wa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran, pia amemtaja Makamu wa Rais wa Marekani J.D Vance kuwa “mbunifu wa makubaliano” ya Iran na Marekani, na kusisitiza kwamba maelezo zaidi ya mapatano hayo yanapaswa kuidhinishwa na Congress ya Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *