s

Chanzo cha picha, Getty Images

Marekani na Iran zimetia saini makubaliano ya awali ya kusitisha vita vya Ghuba, katika juhudi za kumaliza mzozo uliotikisa eneo hilo na kuathiri soko la nishati duniani.

Rais wa Marekani Donald Trump usiku wa kuamkia Jumanne kwa saa za Afrika Mashariki kuwa makubaliano hayo tayari yamesainiwa, ingawa maelezo yake kamili bado hayajawekwa wazi na pande zote mbili zimesema mazungumzo zaidi yanahitajika kabla ya kufikiwa kwa mkataba wa kudumu wa amani.

Makubaliano hayo yanatarajiwa kuongeza siku 60 zaidi za usitishaji vita uliotangazwa mwezi Aprili na pia kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz, ambao Iran imekuwa ikiuzuia tangu mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran mwezi Februari.

Masuala nyeti, ikiwemo mustakabali wa mpango wa nyuklia wa Iran, yanatarajiwa kujadiliwa katika hatua inayofuata ya mazungumzo.

“Makubaliano yamesainiwa kikamilifu,” alisema Trump baada ya kuwasili nchini Ufaransa kuhudhuria mkutano wa viongozi wa mataifa tajiri duniani wa G7.

Pamoja na kusema yametiwa saini Trump akaomngeza Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance anatarajiwa kuhudhuria hafla rasmi ya utiaji saini wa makubaliano hayo mjini Geneva, Uswisi, siku ya Ijumaa.

Habari za makubaliano hayo zilisababisha bei za mafuta duniani kushuka hadi kiwango cha chini zaidi tangu Machi 10, baada ya matarajio ya kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz, njia muhimu inayopitisha karibu asilimia 20 ya biashara ya mafuta duniani.

Mkataba huo unachukuliwa kuwa hatua kubwa zaidi hadi sasa katika juhudi za kumaliza mzozo ambao umeua watu wasiopungua 7,000, wengi wao nchini Iran na Lebanon, huku pia ukiitikisa sekta ya nishati duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *