Mawaziri wa ulinzi wa NATO wanakutana katika Makao Makuu ya NATO huko Brussels. Kikao hiki muhimu cha kazi, kinachoongozwa na Katibu Mkuu Mark Rutte, kinalenga kuimarisha usaidizi kwa Ukraine, tasnia ya ulinzi, na maandalizi ya Mkutano ujao wa Muungano huo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa ulinzi wa Muungano wanatarajiwa kukutana katika Makao Makuu ya NATO huko Brussels mnamo Juni 18, 2026. Vikao vya kazi vitaongozwa na Katibu Mkuu wa muungano huo, Bw. Mark Rutte.

Siku ya Jumatano Katibu Mjuu wa NATO, Mark Rutte, alielezea vipaumbele vya mkutano huo ambao utafanyika leo Alhamisi mjini Brussels. “Washirika wataonyesha maendeleo yao katika kujenga Ulaya yenye nguvu ndani ya NATO yenye nguvu zaidi. Tunahitaji vikosi zaidi, rasilimali zaidi, na msingi imara zaidi wa viwanda. Hii ina maana ongezeko thabiti la uwekezaji wa ulinzi na mgawanyo sawa wa majukumu kwa usalama wa pamoja,” alisema Bw. Rutte.

Kiako hiki kinakuja wakati nchi za Ulaya zikikabiliwa na shinikizo kutoka Marekani kuongeza uwezo wao wa kijeshi na kuunga mkono Washington kufuatia vita vya Iran.

Mwezi Mei, Marekani ilitangaza kuwa haitatoa tena baadhi ya vifaa vya kijeshi vya anga na baharini kwa washirika wake wa Ulaya wakati wa mzozo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuzishinikiza nchi hizo kuongeza matumizi ya ulinzi na kupunguza utegemezi kwa Marekani.

Katibu Mkuu alieleza kwamba, licha ya marekebisho ya michango ya Marekani kwa mfumo wa kikosi cha NATO, Marekani imethibitisha waziwazi kujitolea kwake kwa Muungano huo. “Marekani imepitia ahadi zake, na Washirika wengine wameongeza michango yao,” alisema. “Hiyo ni kweli. Inatufanya tuwe na nguvu zaidi, na hilo ndiyo lengo la NATO 3.0: Ulaya yenye nguvu zaidi ndani ya NATO yenye nguvu zaidi.”

Mkutano wa Kundi la Mipango ya Nyuklia la NATO utafanyika na Washirika husika, ukifuatiwa na kikao cha Baraza la Atlantiki Kaskazini, ambacho kitashughulikia, miongoni mwa mambo mengine, maandalizi ya mkutano wa kilele wa NATO huko Ankara. Mkutano wa Kundi la Mawasiliano kuhusu Ulinzi wa Ukraine, unaoongozwa kwa ushirikiano na Ujerumani na Uingereza, pia utafanyika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *