#HABARI: Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera, Ndugu Faris Buruhani, amewataka vijana mkoani humo kuendelea kulinda amani na utulivu wa nchi.
Amesisitiza kuwa wakati serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikipambana kuwaletea wananchi maendeleo, baadhi ya wapinzani wamebaki kuwaza vyeo na kuchochea uvunjifu wa amani.
Ndugu Faris ameyasema hayo akiwa wilayani Kyerwa, kwenye mwendelezo wa awamu ya pili ya Operesheni ya VIJANA DAKA FURSA NA SAMIA (VIDAFUSA).
Katika mkutano huo, aliwakumbusha vijana kuhusu kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita, ikiwemo mpango wa kuongeza asilimia ya mikopo ya halmashauri kutoka 10% hadi 15% ili kuwainua kiuchumi.
Operesheni hiyo ya VIDAFUSA inayoratibiwa na Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Kagera, inaendelea kupita kwenye kata mbalimbali.
Lengo kuu ni kuhamasisha vijana kuchamkia fursa za kimaendeleo zinazotolewa na serikali, huku wakipuuza siasa za uhasama zinazoweza kuhatarisha mustakabali wa Taifa.
Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
Capitalradio Tanzania
(Feed generated with FetchRSS)