Misri imeandika historia baada ya kupata ushindi wake wa kwanza kabisa kwenye fainali za Kombe la Dunia, ikiifunga New Zealand mabao 3-1 katika mchezo wa Kundi G. Baada ya kuwa nyuma kwa bao 1-0, Mafarao walirejea kwa nguvu kupitia mabao ya Mostafa Zico, Mohamed Salah na Mahmoud Trezeguet.
Misri ilishiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 1934, na kuwa taifa la kwanza kutoka Afrika na ulimwengu wa Kiarabu kufuzu michuano hiyo.
Kufikia mwaka 2026, imecheza fainali za Kombe la Dunia mara nne (1934, 1990, 2018 na 2026), huku ushindi dhidi ya New Zealand ukiwa wa kwanza katika historia yao ya mashindano hayo.

(Feed generated with FetchRSS)