
Jarida la mtandaoni la nchini Somalia, la Hiraan limeripoti kwamba Israel imewatuma wanajeshi wake karibu 50 katika jimbo la Somaliland, miezi kadhaa tangu itanagaze kutambua jimbo hilo lililojitenga na Somalia kama taifa huru.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mtandao wa Hiraan, ulichapisha taarifa hiyo ukimnukuu msemaji wa serikali ya Somalia, ambaye kulingana naye taarifa hiyo imejumuishwa kwenye ripoti ya Intelejensia ya Somalia.
Msemaji huyo amenukuliwa akisema kwamba jeshi la Israel liliwateua wanajeshi wake wenye asili ya kiafrika na hasa Waethiopia, ili kuepuka kuzua maswali na kuwawezesha wanajeshi hao kuingiana na wanajamii kwa urahisi.
Awali shirika la Habari la Reuters liliandika likimnukuu Waziri wa ulinzi wa Somaliland, Mohamed Yusuf Ali, akisema kwamba Israel haina kambi ya kijeshi katika eneo hilo, lakini inasaidia katika kutoa mafunzo kwa polisi na vikosi vya kijeshi.
Waziri huyo aidha alikanusha ripoti kuwa mazungumzo yanaendelea kuhusu Israel kuweka kambi ya kijeshi katika eneo hilo.
Disemba 26 2025, Israel ilikuwa taifa la kwanza duniani na mwanachama pekaa wa umoja wa mataifa kulitambua jimbo la Somaliland kama taifa huru.