Wadau wa elimu nchini wamekuwa wakihoji muda wa kukamilika kwa ujenzi wa vyuo 65 vipya vya mafunzo ya ufundi stadi vinavyojengwa nchini kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 100, ili viweze kuanza kutoa huduma kwa vijana wanaosubiri kujiunga na mafunzo hayo.

Kufuatia hoja hizo, Serikali imesema utekelezaji wa miradi hiyo unaendelea kwa awamu mbalimbali, huku ujenzi ukiwa umefikia wastani wa asilimia 68.

Kwa mujibu wa Serikali, baadhi ya vyuo hivyo vinatarajiwa kukamilika na kuanza kupokea wanafunzi ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *