
Wamarekani wengi wamekatishwa tamaa na serikali yao, wakisema kwamba Waasisi wangesikitishwa sana na hali ya sasa ya kijamii na kisiasa ya Marekani.
Haya ni kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni na shirika la Gallup.
Huku utawala wa Donald Trump ukijiandaa kwa sherehe kubwa ya kuadhimisha Sikukuu ya Robo Karne (Semiquincentennial) ya Marekani – sherehe za kuadhimisha matukio ya kihistoria yaliyopelekea kuundwa Marekani kama jamhuri huru mwaka wa 1776 -, hali ya kukata tamaa wananchi inazidi kuwa dhahiri.
Hafla hiyo, ambayo imepangwa kufikia kilele chake Jumamosi, Julai 4, 2026, ikiadhimisha kumbukumbu ya miaka 250 ya kupitishwa Azimio la Uhuru na kundi la wanachama 56 linalojulikana kama Mababa Waasisi wa Taifa (the Founding Fathers) – linaloongozwa na George Washington, Benjamin Franklin, Thomas Jefferson, Alexander Hamilton na John Adams – inaihiza jamii kufungua tena majeraha ya mgawanyiko wa kimbari, kikabila na kidini unaochochewa zaidi na urais wa Donald Trump.
Utafiti wa Gallup uliochapishwa Jumatano uligundua kuwa ni asilimia 19 pekee ya Wamarekani ndio wanaoamini kwamba kundi lililotia saini Azimio la Uhuru lingekubaliana na mwelekeo wa sasa wa nchi hiyo.
Uchunguzi huo wa maoni unaonyesha kwamba zaidi ya Wamarekani watatu kati ya wanne wanaamini kuwa Waasisi wa Marekani wangekatishwa tamaa na jinsi nchi hiyo ilivyo sasa. Asilimia 77 ya waliohojiwa wamesema waliotia saini Azimio la Uhuru wangekatishwa tamaa na jinsi taifa hilo lilivyoendelea katika kipindi cha miaka 250 iliyopita, huku asilimia 19 wakiamini wangefurahishwa na matokeo.
Utafiti wa Gallup pia umeonyesha kuwa sehemu ya Wamarekani wenye mtazamo hasi kuhusu hali ya sasa ya nchi hiyo imeongezeka kutoka asilimia 71 mwaka 2013 na asilimia 42 mwaka 2001.
Mnamo 1776, Waasisi wa marekanii (the Founding Fathers) walizindua kile walichokiita “Tajiriba Kuu” kuhusu haki za binadamu za Marekani. Lengo lilikuwa kuunda aina ya serikali ya kidemokrasia isiyoegemea upande wa Uingereza, kwa lengo la kuweka misingi ya taifa jipya linaloakisi kanuni za uhuru na usawa.
Hata hivyo kile kinachoonekana sasa na sera za Marekani ni kinyume kabisa na malengo ya Waasisi ambapo nchi hiyo inahusika katika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, mauaji ya watu wasio na hatia, uvamizi dhidi ya nchi nyingine huru, unyang’anyi na uporaji wa rasilimali na utajiri wa mataifa mengine, na baya zaidi kuungana na kushirikiana na utawala katili na wa kifashisti wa Israel unaoendelea kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza huko Palestina na Lebanon.