Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anajua maslahi ya wananchi ndio maana ameridhia kuondolewa tozo na ushuru ambazo zingekuwa mzigo kwao.
Miongoni mwa tozo na ushuru zilizoondolewa baada ya Serikali kufanya marekebisho ni ongezeko la tozo ya pikipiki, ushuru wa kilo ya sukari inayozalishwa ndani na kodi zilizohusu magari yaliyotumika.
“Sababu kubwa ya Serikali kukubali ni kwa sababu wanajali maslahi mapana ya wananchi. Haya ndio maelekezo ya mheshimiwa Rais,” amesema Zungu leo Juni 25, 2026 bungeni jijini Dodoma.
Mbali na hilo, Zungu amesema kulikuwa na kero kwa wafanyabiashara wanaoanza shughuli zao kutakiwa kulipa kodi, lakini Rais Samia ameondoa na watu wafanye shughuli za kwa mwaka mzima kisha walipe.
“Huyu ndiye Rais anayejua maslahi ya wananchi wake. Rais Samia anatambua pikipiki ni chombo muhimu kwa maslahi ya Watanzania ndio maana ameridhia kuondoa ongezeko la kodi (kutoka Sh 95,000 hadi 150,000),”
“Halafu mnasema huko nje Bunge la chama kimoja, halijali maslahi ya watu hasa hili nini? Haya ndio maslahi ya watu,” amesisitiza Zungu.
(Feed generated with FetchRSS)