NAIROBI – Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limethumu mataifa ya kigeni kwa kuendelea kuchochea vita vinavyoendelea nchini Sudan, Amnesty sasa ikitaka jamii ya kimataifa kuchukuwa hatua na kukomesha vita nchini Sudan.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Amnesty katika ripoti yake imetuhumu mataifa ya Flame za Kiraabu, China, Urusi na Ufaransa kwa  kuendelea kufadhili pande hasimu nchini Sudan na hivyo kuendelea kusababisa maafa ya raia.

Ripiti hiyo ilioangazia hali katika mji wa El Fasher, jimbo la Darfur Kaskazini, Amnesty imesema  wapiganaji wa rsf walitekeleza visa ambavyo ni sawa na uhalifu wa kibadamu ikiwemo kuwalenga watu ambao hawana asili ya kiarabu utekaji nyara na  kuwaajiri watoto kupigana vitani.

Amnesty inasema kuendelea kwa vita kunatokana na hali ya kutoadhibiwa kwa wahusika wa uhalifu, jambo linatoa nafasi kwa  pande zinazopigana kuendelea kufanya mashambulizi dhidi ya raia bila kuwajibishwa. Shirika hilo limezitaka nchi zote kuunga mkono uchunguzi wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai (ICC) pamoja na tume za uchunguzi zinazoungwa mkono na umoja wa mataifa na umoja wa Afrika, ili wahusika wafikishwe mahakamani.

Aidha, Amnesty imezitaka nchi zote kusitisha mara moja usambazaji wa silaha na risasi kwa pande zote zinazopigana nchini Sudan. Shirika hilo limesisitiza kuwa Falme za Kiarabu (UAE), ambayo limetaja kuwa msaidizi mkuu wa RSF, haipaswi kupewa silaha zozote hadi itakapoheshimu vikwazo vya umoja wa mataifa.

Kwa mujibu wa Amnesty International, bila hatua madhubuti za kimataifa za kuwawajibisha wahusika na kukomesha usambazaji wa silaha kutoka nje, vita vya Sudan vitaendelea  maafa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *