Muungano wa  Mashirika ya kiraia barani Afrika umezindua kampeni ya kupinga kile unadai mikopo isiyo halali kutoka wakopeshaji  wa kimataifa ,ukitaka umoja wa Afrika kuingilia kati kwa kuja na jopo ambalo litakuwa linashughulikia maswala ya mikopo inayohusu nchi za Afrika.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mashirika haya yakikikutana jijini Nairobi ,yamesema  kuna raia bilioni tatu nukta nne kutoka nchi za Afrika zinazodaiwa madeni makubwa ambao wameathirika kutokana na serikali nyingi kulemewa na mzigo wa kulipa deni hivyo kushindwa kutoa huduma zingine kwa raia.

Dr Samuel Kinyanjui ni mkurugenzi wa shirika la Aids Healthcare Foundation ,ukanda wa Kenya.

“ Kuwe na kikundi cha wanaokopa ‘borrowers’ ambapo nchi zote chini ya AU zinakuwa na kikundi chao kufanya mashauriano na wakopeshaji,ili kukubaliana na kuhusu riba,masharti ya mikopo na ulipaji ili nchi kumudu kulipa mikopo na kushughulikia mahitaji ya nchi. Pesa zinazotokana na akili mnemba au AI asilimia tano zitumike kwenye msamaha wa deni,”alisema Dkt Samuel Kinyanjui.

Aidha mashirika hayo yanatuhumu mashirika ya kimataifa ya kifedha kama vile IMF ,Benki ya dunia kwa kuwekea mataifa ya Afrika riba za juu  na masharti magumu ambayo yanasababishia nchi za Afrika kulipa mara tisa ya kiasa wanachodaiwa.

Baadhi ya sekta ambazo zimeathirika na  ukata wa kifedha ni sekta ya afya haswa miradi ya kupambana na Ukimwi.

Nelson Otuoma anafanya kazi na muungano wa watu wanaoishi na virusi vya HIV nchini Kenya.

“ Serikali inabaki na asilimia 30 pekee yake ,ndiyo inayolipa wafanyakazi,uwekezaji na kujenga hata hospital.Saa hii ukienda kwenye baadhi ya vituo au kaunti zingine ,watakwambia tuna vifaa vya kupima HIV lakini ni kwa ajili ya akina mama waja wazito na makundi maalum,sasa wewe unaenda kwenye vituo binafsi na pengine huna pesa za kulipa ili upimwe virusi,”alisema Nelson Otuoma.

Afrika hulipa hadi dola bilioni 89 kila mwaka kufadhili  madeni ya umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *