Korea Kaskazini imelifanyia jaribio kombora la kimkakati la kruzi na silaha nyingine kutoka katika meli yake mpya ya kivita ya Kang Kon yenye yenye uzito wa tani 5,000 na refu wa mita 140.
Shirika Kuu la Habari la Korea Kaskazini KCNA leo limetangaza kuwa Kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un alisimamia majaribio hayo siku ya Ijumaa.

Majaribio hayo yaliyofanywa na Korea Kaskazini yamejumuisha kombora la mwendo kasi, mizinga ya majini, bunduki za automatiki na mifumo ya kielektroniki ya vita ndani ya meli ya kivita ya Kang Kon.

Kim Jong Un amesema kuwa mazoezi hayo yamekusudiwa lengo likiwa ni kuchunguza na kutihibitisha uwezo wa meli hiyo ya kivita wa kutumia aina mbalimbali za mifumo ya silaha ndani ya meli hiyo ya kivita wakati wa makabiliano.

Baada ya kushuhudia majaribio hayo yaliyofanikiwa, Kiongozi wa Korea Kaskazini  ametaka meli hiyo ya kivita iingizwe katika jeshi la wanamaji la nchi hiyo ndani ya miezi miwili.

Katika hotuba yake kwenye hafla ya kuzindua meli hiyo mwezi Juni mwaka jana, Kim alisema kuwa meli hiyo ya kivita ina “uwezo wa kukabiliana na ndege, meli, nyambizi na makombora ya balistiki.”

Pia alisema kuwa meli hiyo ina uwezo wa kuvurumisha makombora ya kimkakati ya nyuklia na balistiki na kutoa wito wa majeshi ya nchi hiyo kuzidisha juhudi ili kuimarisha uwezo wa kijeshi wa Korea Kaskazini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *