Jeshi la Polisi limewahakikishia Watanzania kuwa hali ya usalama nchini inaendelea kuwa shwari, huku likisema limeimarisha ulinzi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuelekea maadhimisho ya Sikukuu ya Sabasaba, Julai 7, 2026.
Jeshi hilo limesema ulinzi utaimarishwa zaidi katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam pamoja na maeneo mengine ya mikusanyiko ya wananchi, na kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku bila hofu.
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)