Makampuni ya Bakhresa Group yamepongeza maboresho ya Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Sabasaba, huku yakiwahakikishia wateja kuendelea kupata huduma na taarifa kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotolewa katika banda lake.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Bakhresa Group, Rehema Salim amewakaribisha wananchi kutembelea banda hilo ili kujionea bidhaa zote zinazotolewa na makampuni ya Bakhresa Group katika eneo moja, pamoja na kupata ufafanuzi wa huduma mbalimbali kutoka kwa wataalamu waliopo.

✍ Esterbela Malisa
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *