Dar es Salaam. Insta kumepoa sana. Ni Wema pekee wa kupindua meza. Ndiye pekee wa kuamsha dude.

Wema tu anaweza kuifanya Bongo iwe ‘bize’ na mtoto wake katikati ya ‘wordi kapu’. Kwa sasa yupo ‘bize’ na malezi. Ananyonyesha mtoto wake.

‘Mtoto wa taifa’. Kuna Simba na Yanga, kuna CCM na Chadema, kuna Mondi na Kiba. Kuna Wema na maisha ya Wema. Hili ni jeshi la mtu mmoja kwa mishe zake za kusimamisha nchi. Hii siyo kwa kila mtu, hata Mondi kashindwa. Ni Wema pekee. 

Siku hizi washikaji wanapoteza amani kwa sababu ya mapenzi. Bro, usiweke maisha yako yote kwa mtu mmoja mpaka ujisahau. Simama kiume, jenga maisha yako kwanza. Priority iwe pesa, malengo na maendeleo. 

Furaha ya kweli huanza ukipata uwezo wa kuishi unayotaka, si kuishi kwa drama za kila siku.

Ukiwa viwanjani kuna watu wengi hujidai kwa maneno, ama kwa muonekano, lakini mwisho wa siku uwezo wako wa kipesa ndo unaongea.

Usihangaike kuthibitisha wewe ni nani. Jitume, tafuta hela halali, boresha maisha yako, halafu vitu vingine vitafuata vyenyewe. Piga mazoezi kwa afya yako, siyo kwa  kuvutia warembo. Akili, nidhamu’ heshima na ukubwa wa kipato vina thamani kuliko ‘shoo ofu”.

Mambo ni mengi sana mjini siku hizi. Wanamuziki wanajivunia pesa na mali zao, hii na wasanii wa uigizaji pia. Hili jambo kwa sasa ni mtambuka maana hata wakamaria huivunia pesa na mali walizonazo. Wema alikuwa na kila kitu maishani alikosa furaha kwa kutopata mtoto. 

Leo huenda hana alivyokuwa navyo awali, lakini sasa kapewa alichokililia miaka yote nacho ni mtoto. Hivi nataka kusema nini kwani? ‘Ene wei’ mjini kumepoa sana sasa hivi. Arobaini ya mtoto wa taiga Ollie ni lini? Hiyo siku mji utasimamishwa na Madam wema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *