Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, amesema nchi zote za visiwani zilizopiga hatua za maendeleo zimetanguliza utengamano wa kijamii, utawala wa sheria, utulivu wa kisiasa, amani na uwajibikaji.
Othman, ameyasema hayo leo, Alhamisi Julai 9, 2026 alipohutubia hafla ya utiaji saini Tamko la Pamoja la Maridhiano visiwani Zanzibar.
Amesema Zanzibar ina ndoto ya kuwa kituo kikuu cha biashara na usafirishaji, ili kutimiza hayo kunahitaji mfumo imara wa kiuchumi, soko huria, soko la mitaji na mfumo wenye ufanisi wa utatuzi wa migogoro na utoaji haki.
Othman, amesema hatua zinazopaswa kuchukuliwa zisiishie kuwa na manufaa ya kisiasa, bali maslahi ya kijamii, kiuchumi na kiutawala.
Amesema zinapaswa kuwa juhudi za kujenga na kuipeleka mbele Zanzibar ili itimize ndoto zake kwa faida na manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.
(Feed generated with FetchRSS)