Ukurasa mpya wa siasa za maridhiano umefunguliwa Zanzibar baada ya vyama vya CCM na ACT-Wazalendo kusaini tamko la pamoja la muafaka wa kisiasa katika Ikulu ya Zanzibar.

Muafaka huo unalenga kuimarisha amani, utulivu na mshikamano, huku ukiweka msingi wa utekelezaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na kuendeleza mazingira bora ya maendeleo.

Hafla hiyo ya kihistoria ilihudhuriwa na viongozi wakuu wa kitaifa, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *