
Marekani imefanya mashambulizi zaidi dhidi ya Iran kujibu shambulio dhidi ya meli katika Mlango-Bahari wa Hormuz, kamandi kuu ya Marekani kwa Mashariki ya Kati (CENTCOM) imetangaza siku ya Jumamosi jioni.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Vikosi vya Marekani “vimeanzisha mfululizo wa tatu wa mashambulizi dhidi ya Iran wiki hii” baada ya Walinzi wa Mapinduzi ya Iran “kushambulia kwa uwazi meli ya GFS Galaxy, meli ya makontena yenye bendera ya Cyprus” katika Mlango-Bahari wa Hormuz, CENTCOM ilisema, ikiongeza kuwa “moja wa wafanyakazi wa kiraia hajulikani aliko.”
Hayo yanajiri wakati kikosi cha wanamaji cha Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimetangaza leo Jumapili usiku kwamba kimefunga Mlango-Bahari wa Hormuz hadi taarifa zaidi itakapotolewa.
Wakati huo huo Rais wa Marekani Donald Trump ameishutumu Jamhuri ya Kiislamu kwa kupanga njama ya kumuua. Siku ya Ijumaa Rais wa Marekani Donald Trump alitishia “kuangamiza na kuiharibu kabisa” Iran ikiwa serikali ya nchi hiyo itajaribu kumuua. Rais wa Marekani Donald Trump alitishia siku ya Ijumaa, Julai 10, “kuangamiza na kuiharibu kabisa” Iran ikiwa serikali ya nchi hiyo itajaribu kumuua.