#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Chaani na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Ayoub Mohamed Mahamoud Ayoub Mohammed Mahmoud ameitaka Jumuia ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Chaani kuongeza juhudi katika kukabiliana na mmomonyoko wa maadili unaojitokeza katika jamii kwa kushirikiana na wananchi kuanzia ngazi ya mitaa na vijiji kwani hatua hiyo ni msingi muhimu wa kujenga kizazi chenye maadili mema, kulinda mshikamano wa jamii na kuimarisha Chama Cha Mapinduzi

Akizungumza katika kikao cha Baraza Kuu la Wazazi la Wilaya ya Kaskazini A kilichofanyika katika Tawi la CCM Chaani Masingini, Unguja, Mhe. Ayoub alisema changamoto za maadili zinahitaji kushughulikiwa kwa ushirikiano wa viongozi wa chama, wazazi na jamii kwa ujumla, badala ya kuziacha zikikua na kuathiri mustakabali wa kizazi cha sasa na kijacho.

Amesema Jumuia ya Wazazi ina nafasi muhimu katika kujenga na kuimarisha maadili ya jamii kwa kuwa ni moja ya nguzo inayosimamia malezi, hivyo inapaswa kuendelea kutoa elimu na kuikumbusha jamii umuhimu wa kuzingatia misingi ya maadili, heshima, uwajibikaji na uzalendo katika maisha ya kila siku.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
‎Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
‎Capitalradio Tanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *