Wizara ya Katiba na Sheria imefanikiwa kumaliza shauri la madai ya malipo lililowahusisha mkandarasi, kampuni ya Core Multi General Supply Limited na mshirika wake Sehewa Chando ambaye alipewa kazi ya kupiga rangi magari.

Shauri hilo la madai ya Shilingi Milioni 6 limefikia muafaka baada ya mlalamikaji, Sehewa Chando kuongozwa na jopo la wataalamu wa sheria kutoka wizara hiyo juu ya namna bora ya kupata stahiki yake kwa namna ambayo kwa niaba ya kampuni yake, Mkurugenzi wa Core Mult General Supply Limited, Tanziru Mkakile naye ameridhia na wawili hao kukubaliana kutekeleza uamuzi huo.

Wizara ya Katiba na Sheria imetumia Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kutoa huduma za kisheria kwa wananchi na kuwafikia zaidi ya wananchi 1,500.

Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *