Chanzo cha picha, Getty Images
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3
Aston Villa wanamtathmini Pervis Estupiñán, Bruno Guimarães hauzwi, Inter Milan waachana na kumsajili Trevoh Chalobah.
Beki wa kushoto wa Ecuador anayekipiga AC Milan, Pervis Estupiñán mwenye umri wa miaka 28, ni miongoni mwa wachezaji wanaotathminiwa na Aston Villa kwa ajili ya usajili. (Mail)
Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle United wanaamini kuwa kiungo wao wa Brazil, Bruno Guimarães, hauzwi, licha ya tetesi zinazoihusisha Arsenal na mpango wa kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa ada ya pauni milioni 50. (Newcastle Chronicle)
Chanzo cha picha, Getty Images
Inter Milan wameachana na mpango wa kumsajili beki wa England Trevoh Chalobah baada ya kushindwa kumudu ada ya pauni milioni 30 inayotakiwa na Chelsea. Hata hivyo, Como bado wana nia ya kumsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 27. (Corriere dello Sport – in Italian)
Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea wanajiandaa kuwasilisha ofa inayoweza kufikia pauni milioni 21 kwa ajili ya kumsajili beki wa kushoto wa Uhispania wa Rayo Vallecano, Pep Chavarría, mwenye umri wa miaka 28. (Marca – in Spanish)
Chanzo cha picha, Getty Images
Roma wamekataliwa ofa ya euro milioni 40 waliyopeleka kwa Atletico Madrid kwa ajili ya kumsajili Manu Koné, mwenye umri wa miaka 25. Manchester United na Liverpool pia wanamwania beki huyo wa Ufaransa. ((Corriere dello Sport – in Italian)
Aston Villa, Leeds United, Sunderland, Fulham na Brighton zote zinamfuatilia winga wa Sweden mwenye umri wa miaka 20 anayekipiga Barcelona, Roony Bardghji. (Sport via Sport Witness)
Chanzo cha picha, Getty Images
Hull City na Southampton zinaonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Werder Bremen kutoka Ujerumani, Justin Njinmah, mwenye umri wa miaka 25. (Bild – in German)
Kiwango bora alichoonyesha Thomas Schjelderup akiwa na Norway kwenye Kombe la Dunia kimeifanya Benfica kuongeza thamani yake hadi pauni milioni 43. Chelsea, Liverpool na Tottenham Hotspur zote zinamwania winga huyo mwenye umri wa miaka 22. (A Bola – in Portuguese)
Chanzo cha picha, Getty Images
Sporting, Wolves na Southampton zimegonga mwamba katika juhudi za kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Will Lankshear baada ya klabu hiyo kukataa ofa zote zilizowasilishwa. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ameiwakilisha England katika timu za vijana na msimu uliopita alicheza kwa mkopo Oxford United. (Football.London)
Barcelona iko tayari kumuuza kiungo mshambuliaji wa Hispania, Ferran Torres, mwenye umri wa miaka 26, ili kuepuka kulipa takriban pauni milioni 7 kwa klabu yake ya zamani, Manchester City, endapo mkataba wake utaongezwa. (Athletic – subscription required)