Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergei Lavrov, amesema kuwa kuanza tena mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran ni ukiukaji wa Hati ya Makubaliano (MoU) iliyotiwa saini kati ya Tehran na Washington.

Lavrov amesema makubaliano hayo yanapaswa kuheshimiwa na pande zote, akionya kuwa hatua yoyote ya kijeshi inayokiuka vipengele vya mkataba huo inaweza kuhatarisha juhudi za kudumisha utulivu na usalama katika eneo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesisitiza kuwa, mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani dhidi ya Iran yanakiuka Hati ya Makubaliano (MoU) iliyofikiwa kati ya Tehran na Washington. Lavrov amesema hatua hiyo haitachangia kupatikana kwa suluhisho la mzozo uliopo, bali itadhoofisha juhudi za kidiplomasia zilizokuwa zimeanza kuonyesha matumaini.

“Hali hii si tu kwamba haitaleta suluhisho, bali pia inafunga mlango wa fursa ambao ulionekana kufunguliwa kwa kiasi kupitia Hati hiyo ya Makubaliano,” amesema Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Russia.”

Wakati huo huo, Msemaji wa Jeshi la Iran ametoa onyo kali kwa Marekani kuwa hakuna kitendo chochote cha uchokozi kitakachoweza kulazimisha kufunguliwa kwa Lango la Bahari la Hormuz, kufuatia uamuzi wa Tehran wa kulifunga lango hilo la kimkakati baada ya Marekani kukiuka makubaliano.

Brigedia Jenerali Mohammad Akrami-Nia amesema kwamba: “Rais mkandamizaji na fisadi wa Marekani lazima ajifunze kuheshimu sheria za kimataifa, haki za mataifa, na heshima ya watu. Kama tulivyosema hapo awali, Lango la Hormuz halitafunguliwa kamwe kupitia vita, uhasama, au vitendo vya uchokozi vya Marekani.”

Hali hii inajiri wakati Tehran imetangaza kuwa Lango la Hormuz limefungwa “hadi taarifa nyingine” na angalau hadi “mwisho wa uingiliaji kati wa Marekani katika eneo hili.”

Iran imesisitiza mara kwa mara kuwa njia hiyo ya majini haitarejea kamwe katika hali yake ya kabla ya vita na kwamba itasimamiwa na nchi hiyo kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *