Muqawama wa Kiislamu wa Iraq (Islamic Resistance in Iraq) umetangaza zawadi ya dola milioni 10 za Marekani kwa mtu yeyote atakayemuua Rais wa Marekani, Donald Trump.

Hiyo kwa mujibu wa taarifa ziliyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu imesema, hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kauli lilizodai kuwa ni za uchochezi zilizotolewa na Trump dhidi ya makamanda waliouawa katika vita dhidi ya kundi la Daesh (ISIS).

Tangazo la kuweka zawadi kwa atakayemuua Rais wa Marekani, Donald Trump, limekuja kufuatia matamshi yaliyotolewa na Trump kuhusu aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Jenerali Qassem Soleimani, na aliyekuwa Naibu Mkuu wa Vikosi vya Wananchi wa Iraq (Hashd al-Shaabi), Abu Mahdi al-Muhandis, waliouawa. Matamshi hayo yalitolewa wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa Iraq, Ali al-Zaidi, katika Ikulu ya White House.

Hadi sasa, hakuna uthibitisho huru kutoka kwa mamlaka za Iraq au Marekani kuhusu tangazo hilo, na maafisa wa Marekani hawajatoa tamko rasmi kulihusu.

Tarehe 3 Januari 2020, ndege isiyo na rubani ya Marekani ilishambulia msafara wa magari karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq. Shambulio hilo liliua Soleimani pamoja na Abu Mahdi al-Muhandis na watu wengine waliokuwa pamoja nao.

Baada ya shambulio hilo, Rais Donald Trump alitangaza kuwa ndiye aliyeidhinisha operesheni hiyo. Serikali ya Marekani ilidai kuwa Kamanda Soleimani alikuwa akipanga mashambulizi dhidi ya raia na wanajeshi wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati, na kwamba operesheni hiyo ilifanywa ili kuzuia mashambulizi hayo. Iran ilipinga maelezo hayo na kulaani tukio hilo kama ukiukaji wa sheria za kimataifa na wa mamlaka ya Iraq.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *