Katika taarifa, Muungano wa Familia za Mateka na Waliopotea, umesema kuwa agizo la Rais Trump la kusitisha vita mara moja ni muhimu ili kuzuia madhara makubwa na yasiyoweza kurekebishwa dhidi ya mateka.

Trump alikuwa ameitaka Israel kusitisha mashambulizi yake katika eneo hilo la Palestina baada ya Hamas kukubali kuwaachilia mateka wote na kuanza mazungumzo kuhusu mpango wake wa amani.

Hamas iko tayari kwa mazungumzo

Hii leo, afisa mmoja mkuu wa Hamas amesema kundi hilo liko tayari kuanza mazungumzo mara moja ili kukamilisha masuala yote.

Mpango wa Trump uliopendekezwa, unatoa wito wa kusitishwa kwa uhasama, kuachiliwa kwa mateka ndani ya saa 72, kuondoka kwa hatua kwa vikosi vya Israel kutoka Gaza na kupokonywa silaha kwa Hamas.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *