#HABARI: Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwawezesha vijana na wanawake kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 10 isiyo na riba, hatua iliyobadili maisha ya makundi mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Vijana wanane wenye ujuzi wa kuendesha pikipiki, ambao awali walikuwa wakitegemea pikipiki za watu wengine kwa mfumo wa upangishaji, sasa wamefanikiwa kumiliki vyombo vyao kupitia mkopo huo.

Mwenyekiti wa kikundi cha Jitambue Group, Andamazia Mselela, amesema mikopo hiyo imewapunguzia gharama za uendeshaji wa biashara.

Wanufaika hao wamesema mkopo wa Serikali umewapa uhuru wa kupanga matumizi yao, kuboresha kipato na kuachana na utegemezi wa mali za watu wengine.

Katibu wa Jitambue Group, Humphrey Charles, amesema kabla ya kupata mkopo huo walikuwa wakitegemea kazi za vibarua, lakini sasa wana mitaji inayowawezesha kujitegemea.

Mbali na vijana hao, kikundi cha wanawake sita pia kimepata mkopo wa shilingi milioni 32 kwa ajili ya kupanua shughuli zao za biashara.

Kwa upande wake, Afisa Mikopo wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Amina Hassan, amesema katika mwaka huu wa fedha halmashauri imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.91, hatua iliyosaidia kuzalisha ajira na kuwawezesha wananchi wengi kupata mitaji ya biashara bila kulazimika kukopa mikopo yenye riba kubwa.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
‎Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
‎Capitalradio Tanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *