Jeshi la Marekani limesema mashambulio iliyotekeleza wikendi iliopita yalilenga kuiadhibu Iran kufuatia mashambulizi ya Tehran yaliyosababisha vifo vya wanajeshi wake wawili, vifo hivi vikiwa ni vya kwanza kuripotiwa tangu kuanza tena kwa mapigano kati ya pande hizo mbili.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Punde baada ya mashambulizi haya, Iran ilitangaza kuyajibu kwa kulenga kambi mbili za jeshi la Washington huko Kuwait, Tehran ikisema ililenga pia uwanja wa ndege na kituo cha reli.

Mkataba wa awali uliotiwa saini na pande hizo mbili kusitisha vita umevunjika rasmi wakati huu Tehran na Washington zikipambana kila mmoja kujaribu kuwa na udhibiti wa ĂȘneo la Bahari ya Hormuz.

Haya yakijiri, nchi za Kuwait na Bahrain zimesema zinaendelea kuchukua hatua kukabiliana na mashambulio ya Tehran, ambayo imeapa kushambulia mataifa jirani kutokana na ushirikiano wao na Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *