MOROGORO:  CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),kupitia Ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi za Afya kimeendelea kutoa watafiti bora na bobezi wanaofanya mambo makubwa katika kulisaidia taifa na nchi nyingine barani Afrika kwenye kudhibiti magonjwa ya wanyama na yale yatokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

Rasi wa Ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi za Afya ,Profesa Esron Karimuribo amesema hayo akielezea  hatua mbalimbali tangu mwaka 1976  ilipoanzishwa sehemu ya  wanyama chini  Kitivo cha Kilimo Misitu na Sayansi za Afya eneo la Morogoro  kikiwa chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Profesa Karimuribo amesema kuwa  baadhi  ya watafiti  wametangulia mbele ya haki  , Mungu amewaita akiwemo Profesa Rudovick Kazwala aliyekuwa mhadhiri na mtafiti nguli wa Ecosystems na Afya ya Umma ya Wanyama  na  alitambuliwa  mwanasayansi nambari moja nchini Tanzania mwaka 2021.

Amesema mchango mkubwa uliofanywa na ndaki hiyo  ni utafiti wa kuthibiti ugonjwa wa kifua kikuu  kinaenezwa na wanyama  kutokana na kunywa maziwa ambayo hayajachemshwa vizuri ndani yake kuna wadudu  wanaosababisha kifua kikuu kinachokuwa nje ya mfumo wa upumuaji.

‘ Kwa  muda mrefu watu wa sekta ya afya alidhani kuwa kifua kikuu kinaenezwa tu kwa njia ya hew ana katika sehemu hii  tumefanya vizuri” amesema Profesa Karimuribo.

Profesa Karimuribo amesema kupitia Ndaki hiyo  Chuo Kikuu imewezesha kusaidia utafiti wa kudhibiti magonjwa ya mlipuko na moja ya rekondi nzuri ni m waka 2020/2021 baada ya kutokea kwa ugonjwa wa Covid -19 .

Amesema kwa kuwa ugonjwa huo ulikuwa mpya na ulijitokeza ghafla ,Chuo Kikuu kupitia Ndaki hiyo kilikuwa ni kitovu cha watafiti wabobezi ambao walisaidia Maabara ya Taifa kufanya utambuzi wa kwanza wa mama mmoja aliyeingia na ugonjwa huo kutoka nchi za Ulaya.

Profesa Karimuribo amesema kupitia ndaki hiyo imeezesha pia kuwepo mifumo na teknolojia kwa kubuni mfumo unaojulikana Afya ya Msafiri unaorahisisha utendaji kazi maeneo ya viwanja vya ndege kwa utambuzi wa vihatarishi wa magonjwa ya kuambukiza.

Amesema  mafanikio mengine nje ya mipaka , ni  baada ya timu maalumu watafiti  iliyo  kusaidia kudhibiti ugonjwa wa  Covid -19  katika nchi jirani inayopakana na Tanzania baada ya kuombwa.

Profesa Karimuribo amesema mwaka 2023 walipata ombi kutoka  Guinea , Conakry ipatiwe wataalamu ambapo  “yeye” aliongoza kikosi kazi kwenda kuboresha mifumo yao ya kufuatilia magonjwa ya Wanyama kupitia app ya afya data na kuweka katika nchi hiyo na inafanya kazi vizuri.

Amesema Ndaki inapata  wanafunzi wengi kutoka mataifa mbalimbali  yakiwemo ya  Lethoto , Namibia , Madagascar , Burundi , Rwanda , Kenya , Uganda , Sudani na Nchi za Afrika Magharibi  zikiwemo za Nigeria , Bukinafaso  na Ivory Coast

Kwa upande wake mwanafunzi  wa mwaka wa tatu wa  Ndaki hiyo,  Anna Boma  amewaomba  wazazi na jamii iwape fursa  watoto wakike kusoma masomo ya sayansi  shule za sekondari ili yawe ni  daraja  kujiunga na e limu ya juu , na  baadaye waje kuwa wanataaluma bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *