MTWARA: Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi akiwa pamoja na viongozi wengine, ameweka Jiwe la Msingi na kukata utepe kuzindua Mradi wa Ujenzi wa Njia Maalumu ya kusafirisha umeme wa Msongo wa Kilovolti 33 yenye urefu wa kilometa 76 kutoka Kituo cha Switching cha Masasi hadi Wilaya ya Newala, leo Julai 21, 2026, wilayani Newala, mkoani Mtwara.

Mradi huo wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 33 yenye urefu wa kilometa 76 kutoka Kituo cha Switching cha Masasi hadi Wilaya ya Newala umegharimu jumla ya Sh bilioni 4.65, fedha zilizotolewa na Serikali Tanzania.

Kukamilika kwa njia hii mpya ya kusafirisha umeme kumeongeza uthabiti wa mfumo wa umeme, kupunguza changamoto za upatikanaji wa umeme, na kuongeza uwezo wa TANESCO kuhudumia mahitaji yanayoongezeka ya wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji.

Hafla ya uzinduzi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Donald Msengi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. Lazaro Twange, pamoja na wataalam kutoka Wizara na taasisi zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *