
Senegal imetangaza kuwa inaunga mkono harakati za aliyekuwa rais wa nchi hiyo Macky Sall, kuwania nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii imekuja, baada ya Macky Sall kurejea Dakar wiki iliyopita na kukutana na kufanya mazungumzo na rais Bassirou Diomaye Faye.
Kabla ya uamuzi huu, Senegal ilikuwa imekataa kumuunga mkono Sall, ambaye alitawala nchi hiyo kati ya mwaka 2012 hadi 2024 kwa madai ya utawala wake kutekeleza mateso na unyanyasaji mkubwa wa kisiasa alipokuwa madarakani.
Sall amekuwa akiishi nchini Morocco, alikokimbilia tangu alipoondoka madarakani mwaka 2024, na hatua ya kuungwa mkono na rais Faye inaelezwa na wachambuzi wa mambo kuwa ni kwa sababu za kisiasa.
Hii inamaanisha kuwa serikali ya Senegal, sasa itahusika pakubwa, kumpigia debe Macky Sall, anayetaka kuwa Katibu Mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa.
Rais huyo wa zamani alipendekezwa mapema mwaka huu na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, kuwania nafasi hiyo, lakini mataifa zaidi ya 20 ikiwemo Senegal ikikataa kumuunga mkono.