Rais wa Marekani Donald Trump, ameagiza nyongeza ya ushuru kwa asilimia 50 kwa bidhaa mbalimbali zinazoingizwa nchini humo kutoka nchini Canada, hatua ambayo anasema ni ya kulipiza kisasi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Trump amesema amechukua hatua hii akiishtumu Canada kwa kutoza ushuru mkubwa kwa magari, bidhaa za maziwa na pombe kutoka Marekani.

Baadhi ya bidhaa kutoka Canada ambazo Marekani imeongeza ushuru huo ni pamoja na mvinyo na bidhaa kutoka viwandani kama saruji.

Ripoti kutoka Ikulu ya White House, zinasema utekelezwaji wa hatua hii ya Marekani inataanza ndani ya siku 30 zijazo.

Mark Carney, Waziri Mkuu wa Canada, amejibu hatua hii ya Marekani na kusema nchi yake itaendelea kulinda Uchumi wake na itaendeleza mazungumzo na Washington katika siku zijazo, akiongeza kuwa hatua ya Trump inavunja mkataba wa kibiashara kati ya nchi hizo.

Hii sio mara ya kwanza kwa nchi hizo Jirani za Amerika Kaskazini, kujikuta kwenye mvutano wa kibiashara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *