Katika jitihada za kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili kimataifa, Kampuni ya Safal Group inatarajia kuandaa Tuzo za Kiswahili za Safal zitakazofanyika jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kutoa motisha kwa wasomi na wabunifu mbalimbali kuienzi na kuitangaza lugha hiyo duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Alaf Limited, Hawa Bayuni amesema tuzo hizo zitajikita katika vipengele mbalimbali vya fasihi ikiwemo riwaya, ushairi na makusanyo ya hadithi fupi.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *