Hatua mpya inaanza leo Jumamosi, Julai 25, 2026, kwa wafuasi wa Bassirou Diomaye Faye. Muungano wa “Diomaye Rais” unatarajiwa kutoa nafasi kwa chama kipya, kilichotangazwa siku ya Ijumaa, Julai 3, 2026, ambacho jina lake litatangazwa katika mkutano mkuu wa chama hicho. Mkuu wa nchi anatarajiwa kuongoza chama hicho kipya. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Dakar, Juliette Dubois

Chama hiki kipya kinaibuka huku kukiwa na mfululizo wa maafisa kadhaa wa chama cha walio wengi cha PASTEF na chama cha APR wanaovihama vyama hivyo na kujiunga na chama kipya cha Bassirou Diomaye Faye.

Nchini Senegal, jina la chama hiki kipya litatangazwa saa 9:00 alaasiri katika Jumba la Mfalme Fahd. Bassirou Diomaye Faye mwenyewe anatarajiwa kuchukua uongozi wa chama hicho, huku akiendelea, hadi leo, kuwa mwanachama rasmi wa chama cha PASTEF. Chama hiki kipya kwa sasa hakina viti katika Bunge la taifa, ambapo chama cha PASTEF kinashikilia idadi kubwa ya viti.

Hayo yanajiri wakati maafisa wa vyama mbalimbali hususan chama cha walio wengi cha PASTEF na chama cha APR wakiendelea kuvihamakwa kwa wingi vyama hivyo na kujiunga na kujiunga na kambi ya rais. 

Wanachama wawili wa APR waanzisha chama chao

Ndani ya chama cha APR cha rais wa zamani Macky Sall, maafisa wawili hivi karibuni walianzisha chama chao: Thérèse Faye Diouf na Pape Mahawa Diouf. Hakuna hata mmoja wao ambaye amejiunga rasmi na kambi ya rais, lakini kuondoka huku kunaibua maswali kuhusu mustakabali wa mwelekeo wao wa kisiasa.

Kuhusu mkutano mkuu wa chama kipya, ambao awali ulipangwa kufanyika Agosti 8, 2026, sehemu utakaofanyika na tarehe yake vitatangazwa baadaye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *