g

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 2

Real Madrid ina imani kubwa kuwa itafanikisha usajili wa kiungo wa Manchester City, Rodri. Mabingwa hao wa Uhispania wanaendelea na mazungumzo na wanaamini wanaweza kufikia makubaliano ya kumsajili nahodha huyo wa timu ya taifa ya Uhispania mwenye umri wa miaka 30. (Athletic)

Arsenal inafikiria kufanya dili la kubadilishana mchezaji pamoja na fedha ili kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na Argentina, Julian Alvarez. Mpango huo unaweza kumhusisha mshambuliaji wa Sweden, Viktor Gyokeres, mwenye umri wa miaka 28, kuhamia Atletico Madrid.(Cadena Ser – in Spanish)

Roma inamwania winga wa Norway, Oscar Bobb, kutoka Fulham, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kujiunga na klabu hiyo miezi sita tu iliyopita akitokea Manchester City.(Retsport via Football Italia)

Paris Saint Germain bado haijawasilisha ofa rasmi ya euro milioni 120 kwa ajili ya winga wa RB Leipzig, Yan Diomande. Hali hiyo imezipa matumaini Liverpool, Arsenal, Real Madrid na Manchester City, ambazo pia zinamfuatilia nyota huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 19.(Bild – in German)

Kiungo wa Newcastle United, Bruno Guimaraes, anaendelea kuwa lengo kuu la Arsenal katika dirisha hili la usajili. Hata hivyo, kiungo wa Bournemouth, Alex Scott, pia yuko kwenye orodha ya wachezaji wanaotazamwa na klabu hiyo ya London.(Telegraph – subscription required)

Newcastle inatarajiwa kukataa ofa ya pauni milioni 70 kutoka Arsenal kwa ajili ya Guimaraes, ingawa mchezaji huyo anaripotiwa kuwa tayari kuhamia Emirates.(Times – subscription required)

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, anaripotiwa kuwa tayari kuongeza dau hadi pauni milioni 90 ili kuhakikisha anampata Guimaraes.(Mundo Deportivo – in Spanish)

Manchester United haina mpango wa kumuuza nahodha wake Bruno Fernandes, licha ya tetesi zinazoendelea kumhusisha na kuondoka Old Trafford.(Teamtalk)

Como inatarajiwa kufanya mazungumzo na Chelsea kuhusu usajili wa beki Trevoh Chalobah, lakini Chelsea haitamuuza kwa chini ya pauni milioni 30.(Sky Italia – in Italian)

Chelsea pia imewasilisha ofa ya awali kwa winga wa Bayer Leverkusen, Kerim Alajbegovic, mwenye umri wa miaka 18.(Kicker – in German)

Arsenal na Hamburg zinaendelea na mazungumzo kuhusu kiungo wa Ureno, Fabio Vieira, ambaye anataka kujiunga na klabu hiyo ya Bundesliga baada ya kucheza kwa mkopo msimu uliopita.(Florian Plettenberg)

Wakati huo huo, mshambuliaji wa England, Marcus Rashford, amealikwa kushiriki katika makala maalumu ya Amazon kuhusu Manchester United, hatua inayotafsiriwa kuwa viongozi wa klabu hiyo bado wanataka aendelee kubaki Old Trafford.(Mirror)

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *