Uchumi wa Mkoa wa Shinyanga umetajwa kuongezeka kwa asilimia 22 katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2025, huku pato la wastani la mtu mmoja likiongezeka kutoka shilingi milioni 1.86 hadi shilingi milioni 1.99, sawa na ongezeko la asilimia saba.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi Juni 2026.

Amesema uchumi wa mkoa umeongezeka kutoka shilingi bilioni 7.5 hadi shilingi bilioni 9.2. Aidha, zaidi ya vikundi 900 vya vijana vimenufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri katika kipindi hicho kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi na kuongeza fursa za ajira.

Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *