Abbas Araghchi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema makubaliano kati ya Iran na  IAEA  ya mwezi Septemba huko Cairo hayana tena nafasi.

Tehran ilimlaumu mkuu wa shirika hilo Rafael Grossi kwa kutoa taarifa zilizokinzana ambazo wanadai zilipelekea mashambulizi ya Israel na Marekani mwezi Juni mwaka huu.

Hivi majuzi, mataifa makubwa ya magharibi yalichukua uamuzi wa kuiwekea tena vikwazo Iran  yakitaja kuwa nchi hiyo imeshindwa kutoa ushirikiano kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *