Huko nchini Madagascar waandamanaji walimiminika jana katika mitaa ya mji mkuu Antananarivo wakimtaka rais  Andry Rajoelina  kujiuzulu, harakati ambazo rais huyo amezitaja kuwa jaribio la mapinduzi. Umoja wa Mataifa umesema hadi sasa watu 22 wameuawa huku mamia ya wengine wakijeruhiwa.

Nchini Morocco, vijana waliandamana kwa siku ya nane mfululizo hapo jana wakidai uwepo wa huduma bora za afya na elimu. Hivi majuzi maandamano hayo yaligeuka kuwa ya vurugu na kusababisha vifo vya watu wawili huko Agadir, kitendo kilichozidisha hasira ya waandamanaji katika  taifa hilo la Kifalme.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *