Hatua hizi za M23 zinachukuliwa hasa wakati huu makubaliano ya amani yakishindwa kutekelezwa ipasavyo huko mashariki mwa  Kongo . Kundi hilo linaloungwa mkono Rwanda kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, limekuwa likiajiri maafisa na kutoza kodi, kutoa mafunzo kwa majaji, wanajeshi na polisi katika jitihada za kutengeneza utawala uliyo sambamba na uongozi wa serikali ya Kinshasa.

Eneo la mashariki mwa DRC  lenye utajiri mkubwa wa madini limekumbwa na migogoro kwa zaidi ya miongo mitatu na kusababisha maafa makubwa. Mgogoro uliongezeka baada ya kuibuka tena kwa M23 mwaka 2021 ambapo mapema mwaka huu kundi hilo lilichukua udhibiti wa miji muhimu ya Goma na Bukavu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *