Imeelezwa kuwa shughuli za kibinadamu zinazofanyika ndani na kandokando ya Hifadhi ya Ziwa Victoria zimeanza kuathiri kwa kiwango kikubwa ustawi wa samaki na mazingira yao ya kuzaliana.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Dkt. Iman Kikoti, amesema miongoni mwa shughuli hizo ni kilimo, ambapo baadhi ya wakulima hutumia dawa za viwandani kwenye mashamba yao. Dawa hizo husafirishwa na maji ya mvua na kuingia zwani, jambo linalochafua maji na kuharibu mazalia ya samaki.
#AzamTVUpdates
✍Ester Sumira
Mhariri | John Mbalamwezi