
Msemaji wa harakatin ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS amesema kuwa, Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa haikuwa vita tu vya kuwashinda wavamizi, bali ni hatua ya mabadiliko ambayo ilifichua sura halisi ya wavamizi hao na kuwatenga.
Fawzi Barhoum, msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu na kiongozi mwandamizi wa Hamas, alisema hayo Jumanne ya jana katika kumbukumbu ya mwaka wa pili wa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqswa na kubainisha kwamba, operesheni hiyo ni mwanzo wa kuhesabika wa kufikia tamati uvamizi na ukaliaji mabavu duniani.
Msemaji huyo wa HAMAS amesema kuwa, uungaji mkono wa wananchi kwa muqawama huo ni jabali lililosambaratisha mipango ya wavamizi hao na kwamba, Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqswa ni jibu la kihistoria kwa njama hizo za kuangamiza kadhia ya Palestina pamoja na malengo yake matukufu.
Jumanne ya jana Oktoba 7 ilisadifiana na kutimia miaka miwili tangu Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ilipotekeleza operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa na kutoa pigo kubwa na la kihistoria dhidi ya utawala haramu wa Israel.
Operesheni ya kimbunga cha al-Aqsa ilifanyika katika eneo la mpaka kati ya Ghaza na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel. Operesheni hiyo ilianza wakati wa alfajiri. Vikosi vya Hamas kwanza walipiga maeneo ya Wazayuni kwa kutumia maroketi na walirusha makombora 5,000. Baada ya hapo, walivuka ukuta uliojengwa na jeshi la Israel na kuingia kwenye maeneo ya walowezi wa Kizayuni. Zaidi ya wanajeshi 1,400 wa Israel waliangamizwa na 3,500 wengine walijeruhiwa kwenye operesheni hiyo ya kishujaa.