Waziri wa Mambo ya Nje ametoa mjibizo kwa kauli za hivi karibuni za Rais wa Marekani kuhusu mpango wa nyuklia wa Jamhuri ya Kiislamu na kueleza kwamba: Wamarekani wataabani kuingia vitani kupigana kwa ajili ya “vita visivyo na mwisho” vya Israel.

Sayyid Abbas Araqchi ameeleza hayo kwenye mtandao wa kijamii wa X akijibu matamshi yaliyotolewa hivi karibuni ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na kuandika: “Nilipoondoka kuelekea kwenye duru ya tano ya mazungumzo na Bwana Witkoff tarehe 2 Juni, niliandika:

Silaha za nyuklia sifuri = tuna makubaliano.

Urutubishaji urani sifuri = hakuna makubaliano yoyote.

Laiti kama Rais wa Marekani angeangalia dondoo za mazungumzo haya, ambazo zilirekodiwa na kuusajiliwa na mpatanishi, angeweza kuona jinsi tulivyokuwa karibu na kusherehekea makubaliano mapya na ya kihistoria ya nyuklia”.

Araghchi ameendelea kuandika: “Rais wa Marekani anapaswa akumbuke kuwa, hakukuwepo na ‘taarifa’ zozote kwamba Iraq ilikuwa imeficha silaha za maangamizi makubwa. Lakini kitu pekee kilichotokea ni uharibifu usiotasawirika, kuuawa maelfu ya Wamarekani, na kupotea bure dola trilioni saba za fedha za walipa kodi wa Marekani”.

Katika sehemu nyingine ya andiko lake hilo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: “vile vile, hakuna ‘taarifa’ yoyote inayoonyesha kwamba, kama Israel isingeihadaa Marekani kuwashambulia kijeshi wananchi wa Iran, Iran ingekaribia “ndani ya mwezi mmoja” kutengeneza silaha ya nyuklia. Baada ya kushindwa operesheni hiyo, Israel sasa inajaribu kuchora tishio la kufikirika kuhusu nguvu za kiulinzi za Iran. Wamarekani wataabani kuingia vitani kupigana kwa ajili ya “vita visivyo na mwisho” vya Israel.

Araghchi amemalizia andiko lake hilo kwa kueleza kwamba, Iran ni nchi “kubwa” na Wairani ni taifa “kubwa” na warithi wa ustaarabu “mkubwa” wa kale. Yamkini majengo na mashine yakaangamizwa, lakini hilo halitaweza “katu” kutia doa irada na utashi wetu. Kuzidi kung’ang’ania kosa hili la kimahesabu hakutatatua tatizo lolote. Hakuna njia yoyote ya utatuzi isipokuwa kufikia “suluhisho la mazungumzo”…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *