Mjumbe mkuu wa Hamas Khalil Al-Hayya amesema siku ya Jumanne wakati wa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Israel nchini Misri kwamba kundi hilo “linataka kuhakikishiwa kutoka kwa Rais wa [Marekani] Donald Trump na nchi fadhili kwamba vita vitaisha mara moja na kwa wote”.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Hatuna imani na ukaliaji wa maeneo ya Gaza, hata kwa sekunde moja,” ameambia vyombo vya habari vya Misri Al-Qahera News, akimaanisha Israel.

“Ukaliaji wa Israel, katika historia yake yote, haitimizi ahadi zake, na tumeona hili mara mbili katika vita hivi. Kwa hiyo, tunataka hakikisho la kweli,” ameongeza, akiishutumu Israel kwa kukiuka usitishaji mapigano mara mbili katika mzozo wa sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *