Kurejeshwa nyumbani kwa wakimbizi, ni miongoni mwa mambo saba muhimu yaliyokubaliwa kwenye mkataba wa Washington kati ya serikali ya Kinshasa na Kigali, kusaidia kuleta amani ya kudumu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Je, makubaliano hayo yanatekelezwa ?

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, serikali ya DRC, Rwanda na waasi wa AFC/M23 wanapaswa kuhakikisha kuwa wakimbizi wote wanakuwa salama, na wanarejea katika nchi walizotokea, kwa hiari na kwa amani.

Namna ya utekelezwaji wa suala hili, bado linasalia tata, kwenye mazungumzo ya Doha, hasa kati ya serikali ya DRC na waasi wa AFC/M23, lakini pia kati ya Kigali na Kinshasa.

Kwanza, kuna swali la idadi ya wakimbizi wanaotakiwa kurudi nyumbani. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, Rwanda inawahifadhi wakimbizi 137,000 waliokimbia machafuko nchini DRC na Burundi, ambapo 80,000 ni Wakongomani.

Changamoto kubwa kwa serikali ya DRC ni kuwatambua wakimbizi hao, na imeendelea kusisitiza kuwa, haina takwimu kamili.

Jambo lingine ni kwamba, Kamati maalum ya kushughulikia namna wakimbizi hao watakavyorejea katika nchi zao, haijaundwa.

Mwisho, suala lingine tata ni msimao wa serikali ya DRC kuwa wakimbizi hao hawawezi kurejeshwa katika maeneo ambayo bado yana vita, na wanaweza kurejea tu baada ya mkataba wa mwisho kupatikana na vita kusitishwa kabisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *