
Baraza la mawaziri la Israel limepangwa kukutana leo Alhamisi saa kumi na mbili jioni (saa za Israel) kujadili “mpango wa kuachiliwa huru kwa mateka wote wa Israel,” kulingana na taarifa rasmi kufuatia Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka huko Gaza.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na ajenda ya mkutano iliyotolewa na serikali kwenye tovuti yake, mpango huo utawasilishwa kwa wajumbe wa baraza la mawaziri na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
Rais wa Marekani alitangaza usiku wa Oktoba 8 kuamkia Oktoba 9 kwamba Israel na Hamas wameidhinisha awamu ya kwanza ya mpango wake wa amani. Kutiwa saini rasmi kwa makubaliano hayo kumepangwa Alhamisi, Oktoba 9, na kunahusika na kuachiliwa huru kwa mateka wote wa Israel ambao bado wanashikiliwa katika Ukanda wa Gaza.
Misri inapongeza “wakati muhimu” kufuatia tangazo la makubaliano ya Gaza
“Huu ni wakati muhimu katika vita vya Gaza,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Badr Abdelatty aersema katika taarifa yake, akibainisha kwamba waziri wa mambo ya nje wa Misri atasafiri kwenda Paris leo Alhamisi kwa mkutano wa mawaziri “kujadili mipango kuhusu hali” katika ardhi ya Palestina iliyoharibiwa na zaidi ya miaka miwili ya vita.
Emmanuel Macron anakaribisha “matumaini makubwa” kufuatia makubaliano kati ya Israel na Hamas
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekaribisha “matumaini makubwa” yaliyotolewa na makubaliano kati ya Israel na Hamas na kueleza matumaini kwamba yataruhusu “kufunguliwa kwa suluhu la kisiasa kwa msingi wa suluhisho la serikali mbili.” “Ufaransa iko tayari kuchangia lengo hili. Tutajadili alasiri hii mjini Paris na washirika wetu wa kimataifa,” ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, akimaanisha mkutano utakaofanyika kujadili mbinu za baada ya vita.