Afisa mmoja mkuu wa shirika hilo Mohammed al-Mughayyir, amesema magari ya jeshi la Israel pia yameondoka kutoka maeneo ya mji wa kusini wa Khan Yunis lakini mapigano bado yanaendelea.

Mughayyir amesema milio ya risasi inasikia hadi sasa na kwamba jeshi hilo pia limelenga wafanyakazi wa baraza la manispaa la Gaza kaskazini mwa kitongoji cha Sheikh Radwan mjini Gaza City.

Moshi mkubwa waripoti kufuka kaskazini mwa Gaza

Mughayyir pia amesema  mfanyakazi mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi na jeshi hilo la Israel huku mwanamume mmoja akiuawa mjini Khan Yunis .

AFP imeripoti kufuka kwa moshi mkubwa kutoka kaskazini mwa Gaza leo asubuhi.

Kwa upande wake, jeshi la Israel limesema kuwa linafuatilia ripoti hizo ya mashambulizi katika ukanda wa Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *