
Waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso Karamoko Jean-Marie Traore, amesema nchi hiyo imekataa kushurutishwa na Marekani.
Katika taarifa kupitia televisheni ya taifa, waziri Jean-Marie Traore amesema wanalichukulia pendekezo hilo kuwa lisilofaa na linaloenda kinyume kabisa na kanuni ya utu.
Huduma za visa za Marekani zahamishiwa Lome
Mapema, ubalozi wa Marekani katika mji mkuu Ouagadougou, ulitangaza kusitishwa kwa huduma za kawaida za viza nyingi za watu wanaoishi Burkina Faso.
Badala yake raia wa nchi hiyo watahitajika kutafuta huduma hizo mjini Lome, mji mkuu wa taifa jirani la Togo.
Juu ya hatua hiyo, Waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Jean-Marie Traore ameikosoa na kuhoji ikiwa ni njia ya kuliwekea shinikizo taifa hilo alilolitaja kuwa eneo lenye hadhi.